20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Rita ajitoa kwenye The X Factor

RitaLONDON, ENGLAND

JAJI kiongozi katika shindano la The X Factor la kuibua vipaji vya wasanii nchini Uingereza, Rita Ora, ametangaza kujitoa katika kundi hilo baada ya kulitumikia kwa mwaka mmoja.

Inadaiwa kwamba mrembo huyo aliyefanya mashindano ya The X Factor msimu uliopita kuwa na mvuto mkubwa, lakini juzi aliweka wazi kupitia akaunti yake ya Twitter kwamba amejitoa katika kazi ya ujaji.

Jaji huyo amesema ameondoka katika kundi hilo baada ya kuwaona majaji wenzake, Cheryl Fernandez na Nick Grimshaw, wakiondoka mapema mwaka huu.

“Nitumie nafasi hii kuwashukuru wote ambao walikuwa wanafuatilia kazi zangu tangu nilipojiunga mwaka jana, namshukuru sana kiongozi wangu Simon Cowell kwa kunipokea na kusimamia kazi zangu.

“Nitafurahi kuiona The X Factor ikifika mbali zaidi, nitawakumbuka sana majaji wenzangu niliowaacha na watu wengine, naweza kurudi siku yoyote,” aliandika Rita kwenye akaunti yake ya Twitter.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles