RIHANNA, DJ KHALED KUBURUDISHA TUZO ZA GRAMMY

0
772

LOS ANGELES, Marekani


WANAMUZIKI Rihanna na Dj Khaled wamepewa ‘shavu’ la kupanda jukwaani na kutumbuiza katika hafla ya utoaji Tuzo za Grammy.

Mbali na wawili hao, pia waandaaji wa tuzo hizo zitakazotolewa mwezi huu, wamemtaja rapa Bryson Tiller.

Tayari mashabiki wa Rihanna na Dj Khaled wanasubiri kuona watakavyowapagawisha kwa ngoma yao ya ‘Wild Thoughts’ ambayo waliiachia miezi michache iliyopita.

Wasanii wengine watakaopanda jukwaani siku hiyo ni Cardi B, Bruno Mars, Kesha, SZA, Luis Fonsi na Daddy Yankee.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here