26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAWAKILI WAUKATAA USHAHIDI WA VIDEO KESI YA LEMA

 

Na JANETH MUSHI

-ARUSHA

Ushahidi wa video katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), umeshindwa kuwasilishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha, baada ya mawakili wa utetezi kuwasilisha pingamizi la kuiomba mahakama hiyo kutopokea ushahidi huo.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Devotha Msoffe Wakili wa Utetezi, John Mallya na Sheck Mfinanga waliiomba mahakama isipokee vielelezo kwa sababu shahidi aliyeomba vielelezo hivyo vipokelewe mahakamani hapo hakuandaa yeye.

Shahidi wa sita, Inspekta Aristides Kasigwa wa Idara ya uchunguzi ya kisayansi Makao Makuu ya Upelelezi Dar Es Salaam, aliiomba mahakama hiyo ipokee ushahidi wa video.

Mahakama hiyo imeahirisha kesi hiyo hadi Februari 16 mwaka huu, ambapo itatoa uamuzi wa pingamizi hilo la mawakili wa utetezi.

Katika kesi hiyo ya uchochezi namba 440 ya mwaka 2016, Lema anadaiwa kutoa lugha za uchochezi katika mkutano uliofanyika Oktoba 22 mwaka juzi, maeneo ya Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro Jijini Arusha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles