25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WOLPER: UFUNDI SEREMALA UNANILIPA

NA JESSCA NANGAWE


MSANII wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper, amesema mbali na sanaa yake hiyo, amekuwa akipata hela nzuri kupitia kazi yake ya mitindo ambapo sasa ameamua kuwa fundi seremala.

Wolper amesema huu ni wakati wake wa kutengeneza fedha ili kutimiza ndoto zake za kuishi maisha aliyojipangia tangu akiwa mdogo.

“Hakuna asiyependa maisha mazuri na tutambue tu hayaji kirahisi zaidi ya kujituma usiku na mchana kuhakikisha unaweka mambo yako sawa, sasa hivi nimewekeza zaidi kwenye mitindo na kama mnavyoniona kazi yangu ya useremala inanilipa sana, nashukuru Mungu hiki ninachokipata,” alisema Wolper.

“Unatakiwa upende hela yako, usitambe na hela ya mwanamume, usitambe na hela ya kupewa, fanya kazi yako ikupe heshima,” amesisitiza Wolper.

Ray, Chuchu waanika sura ya mtoto wao

NA JESSCA NANGAWE

MTOTO wa mastaa wa filamu hapa nchini, Ray Kigosi na Chuchu Hans aitwaye Jayden, ameonyeshwa sura kwa mara ya kwanza jana baada ya kutimiza mwaka mmoja tangu azaliwe.

Mtoto huyo jana alitimiza mwaka mmoja huku wazazi wao kila mmoja akimtakia heri sambamba na mastaa mbalimbali.

Ni mwaka sasa mtoto huyo amekuwa akifichwa sura na wazazi wake, huku wakiahidi kumwonyesha baada ya kutimiza mwaka.

Mama wa mtoto huyo, Chuchu Hans, alionyesha furaha yake na kusema hana cha zaidi ya kumshukuru Mungu kwa zawadi hiyo kwa kuwa amepitia mambo mengi hadi kufanikiwa kumpata mtoto huyo.

“Nilipitia kipindi kigumu sana mpaka kumpata Jayden, mimba zaidi ya tatu zilitoka na niliumia sana ingawa huyu si mtoto wangu wa kwanza, namwomba Mungu anikuzie mtoto huyo na aweze kutimiza ndoto zake,” alisema Chuchu Hans.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles