25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

JAY Z: BADO NINA DENI KWENYE MUZIKI

LAS VEGAS, Marekani


MKALI JAY Z amefichua kwamba, hafikirii kuachana na muziki kwa kuwa bado hajafikia malengo aliyojiwekea kabla ya kukaa pembeni.

Staa huyo anayetamba na albamu yake ya 4:4:4 ambayo inafanya vizuri sokoni kwa sasa, alidai kuwa mbali na mafanikio, muziki uko kwenye damu yake, hivyo huenda ikamchukua muda kuachana nao.

“Nataka kuendelea kufanya vizuri kadiri nitakavyoweza. Nina mipango mingi, zaidi ni kufurahia kazi nzuri na si kupata fedha,” alisema rapa huyo.

Itakumbukwa kuwa kutoka kwa albamu yake hiyo kuliambatana na kuibuka upya kwa bifu lake na swahiba wake wa zamani, Kanye West.

Lakini pia, ni baada ya albamu hiyo ndipo Jay Z mwenyewe alipofichua kuwa aliwahi kumsaliti mkewe, Beyonce.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles