26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Rihanna atikisa kwa utajiri, awafunika Beyonce, Madona

NEW YORK, MAREKANI

SIKU moja baada ya rapa Jay Z, kutangazwa kuwa bilionea wa kwanza katika muziki wa hip hop, staa wa muziki wa RnB, Robyn Fenty maarufu kwa jina la Rihanna, ameingia kwenye historia mpya ya kuwa msanii wa kwanza tajiri kwa upande wa wanawake.

Wasanii wengi wamekuwa wakijikusanyia pato kubwa mara baada ya kuachia albamu au nyimbo ambazo zitafanya vizuri kwenye chati mbalimbali za muziki duniani, lakini imekuwa tofauti kwa Rihanna.

Mara ya mwisho kwa Rihanna kuachia wimbo mmpya ilikuwa Januari 27, mwaka 2016, ambapo wimbo huo ulijulikana kwa jina la Anti, uliachiwa chini ya uongoz wa Roc Nation ambao unamilikiwa na rapa Jay Z.

Mbali na kukaa muda mrefu bila ya kuachia wimbo au albamu, Rihanna kwa mujibu wa Jarida la Forbes ameingiza kiasi cha dola milioni 600, ambazo ni zaidi ya trilioni moja za Kitanzania.

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 31, amekuwa akiingiza kiasi hicho cha fedha kutokana na kazi zake za muziki, ikiwa pamoja na ziara mbalimbali siku za hivi karibuni na biashara yake ya bidhaa za urembo.

Wasanii ambao Rihanna anashindana nao kwa sasa ni pamoja na Madonna ambaye anakadiriwa kuwa na kiasi cha dola milioni 570, Celine Dion dola milioni 450 na mke wa Jay Z, Beyonce mwenye utajiri wa dola milioni 400.

Mwezi mmoja uliopita, Rihanna alifanya mazungumzo na The New York Times, aliweka wazi kuwa, anapambana kwa kufanya kazi zingine ambazo hatamani kuzifanya, lakini ikiwa ni lengo la kuutafuta utajiri.

“Fedha zipo njiani, lakini nimekuwa nikifanya kazi mbalimbali ambazo zingine sizipendi kuzifanya lakini kwa ajili ya kuutafuta utajiri,” alisema Rihanna.

Wimbo wa Anti, unatajwa kuwa miongoni mwa chachu ya ongezeko la kipato chake, inadaiwa kwamba wimbo huo unaongeza mauzo ya biadhaa zake za urembo. Alianza kujiingiza moja kwa moja kwenye biashara ya urembo mwaka 2017 na ikaanza kupenda na idadi kubwa ya wanawake.

Mapema mwaka huu, kampuni ya LVMH Moet Hennessy Louis Vuitton, ambayo inatajwa kuwa moja kati ya kampuni zinazotengeneza bidhaa mbalimbali za urembo, iliingia mkataba wa kufanya kazi na Rihanna ambapo msanii huyo anachukua kiasi cha dola milioni 10 kupitia kampuni hiyo.

Lakini mbali na mafanikio hayo, mashabiki wake wametumia mitandao ya kijamii wakimuomba aachie wimbo mpya au albamu ili waweze kupata burudani kwa kuwa muda mwingi sasa anautumia kwa ajili ya biashara ya vifaa vyake vya urembo.

Mwishoni mwa mwaka jana, msanii huyo aliweka wazi kuwa, yupo kwenye mpango wa kuachia albamu mpya ambayo itakuwa ikijulikana kwa jina la R9, lakini hajaweka wazi ataiachia lini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles