Na Mwandishi Wetu – Chalinze
MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete (CCM), ameahidi kuwanunulia kombati vijana zaidi ya 400 wanaotarajia kumaliza mafunzo ya jeshi la akiba jimboni humo.
Akizungumza mjini hapa jana, alisema vijana hao watapata ajira kupitia mashirika mbalimbali yaliyopo wilayani Bagamoyo.
Aliwahakikishia vijana hao kuwa watakapomaliza mafunzo hayo Serikali itahakikisha wanapatiwa ajira katika sehemu mbalimbali ili iwe fundisho kwa wale wanaoyabeza.
Pia alisema Serikali imewafungulia milango ya kutosha vijana kupitia fursa mbalimbali zinazopatikana ili wanufaike na nchi yao.
Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.