24.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Majaliwa atoa siku 25 kwa watumishi Chamwino

Na Mwandishi Wetu – Dodoma


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku 25 kwa watumishi wa Halmashauri ya Chamwino wanaoishi nje ya kituo chao cha kazi wawe wamehamia.

Pia amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Vumilia Nyamoga orodha ya watumishi hao wanaoishi nje ya kituo cha kazi kwa hatua zaidi.

Agizo hilo alilitoa mjini hapa jana wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na ofisi ya DC wa Chamwino.

“Ifikapo Desemba 15, mwaka huu watumishi wote wawe wamehamia katika kituo chao cha kazi. Sheria ya utumishi inamtaka mtumishi aishi katika maeneo ya kituo cha kazi,” alisema.

Pia alisema lazima watumishi wote wa umma wafuate sheria, kanuni na taratibu za utumishi na atakayeshindwa kuhamia atakuwa amejiondoa katika utumishi.

Aliwataka watumishi wa halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wakuu wa idara na madiwani watambue vyanzo vyote vya mapato.

Alisema baada ya kuvitambua wasimamie utaratibu wa ukusanyaji kwa njia ya kielektroniki ili kuiwezesha halmashauri kupanga miradi na kuitekeleza kupitia fedha za ndani.

Pia alikagua barabara za mitaa katika mji wa Chamwino zenye urefu wa kilomita 3.5 zinazojengwa kwa kiwango cha lami na kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo.

Baada ya kukagua barabara hizo, alikagua ujenzi wa miundombinu ya majengo ya Kituo cha Mabasi Chamwino na kisha kuzungumza na wananchi waliofika  kituoni hapo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,074FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles