23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rehmtula, Kinondoni waungana kuadhimisha kumbukizi ya Baba wa Taifa

NA MWANDISHI WETU

MBUNIFU wa mavazi Ally Rehmtula kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni, ameandaa onyesho la mavazi katika tamasha la ‘Sunset Festival’ kwa wahitimu ambao alikuwa akiwapatia mafunzo kwa miezi mitatu litakalofanyika Oktoba 14,2021 kwenye fukwe za Coco.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema katika onyesho la Sunset Festival, nguo zitakazoonyeshwa zimetengenezwa na wanafunzi wake tisa ambao amekua akiwapatia mafunzo.

“Nimekuwa na darasa kwa vijana ambao wanapenda kuwa wabunifu huu ni msimu wa pili wa mafunzo haya, katika shoo ya Sunset Festival, mavazi ambayo yataonyeshwa yametengenezwa na wahitimu hao ambapo pia watatunukiwa vyeti vyao.

“Tunafanya usaili kwa wanamitindo wa kike na kiume kwa ajili ya kuonyesha mavazi hayo na majaji watakuwa wahitimu wenyewe kwa sababu wao wanafahamu wanataka watu wa aina gani,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles