28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

REDIO 5 KURUDI HEWANI DESEMBA 16

Mkurugenzi  wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi.
Mkurugenzi wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi.

Na Mwandishi Wetu – ARUSHA

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jana imefanya ukaguzi wa mwisho kujiridhisha na kuruhusu kituo cha utangazaji cha Redio 5 cha jijini hapa kurudisha  matangazo yake hewani Desemba 16.

Akizungumza na wafanyakazi wa redio hiyo, Mkurugenzi  wa Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Fredrick Ntobi, alisema wao kama mamlaka waliamua kufanya ukaguzi kujiridhisha ili kurudisha matangazo ya kituo hicho hewani Desemba 16 ambayo ndiyo siku rasmi ya kumalizika kwa adhabu waliyopewa.

Alisema mamlaka hiyo ilifanya ukaguzi wa studio ya kurusha matangazo, kuzalisha vipindi, chumba cha habari, ofisi zote za kituo na mnara wa kurushia matangazo na kote walikuta kila kitu kiko sawa kwa kazi kama mamlaka inavyotaka.

“Niwakumbushe watangazaji na waandishi  kufuata maadili ya uandishi wa habari ili kulinda vituo vyenu na taaluma zenu kwa ajili ya kuendelea kuhabarisha na kuelimisha jamii nzima ya Watanzania,” alisema Ntobi.

Naye Mkurugenzi wa Tan Communication Media inayomiliki kituo hicho cha redio, Robert Francis, aliwataka wasikilizaji wa redio hiyo kukaa mkao wa kuhabarika, kupata burudani na kuelimika zaidi kwani wamejipanga kurudi hewani kwa kishindo.

“Mimi niwaombe wasikilizaji wetu ambao  najua wametu-miss, wakae tayari kwa kuhabarika, kingine niwape pole wasikilizaji  wetu wote kwa kutosikika hewani kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja na wadau ambao tumekuwa tunashirikiana katika mambo mbalimbali kwani tunarudi rasmi Desemba 16,” alisema Francis.

Septemba 16, mwaka huu kituo hicho kilisimamishwa kurusha matangazo yake na TCRA kwa muda wa miezi mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles