24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

JAJI MKUU AWAONYA MAWAKILI

JAJI Mkuu, Mohammed Othman Chande
JAJI Mkuu, Mohammed Othman Chande

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

JAJI Mkuu, Mohammed Othman Chande, amesema ndani ya mwaka mmoja wamepokea malalamiko 71 kuhusu mawakili, yakiwamo ya kutoa siri za wateja.

Hayo yalisemwa jana katika hafla ya kuwaapisha mawakili wapya 287. Idadi hiyo imefikisha jumla ya mawakili kufikia 6,082.

“Idadi ya mawakili imefikia 6,082. Idadi hiyo inahitaji kuongezeka, mawakili wanatakiwa kuwa na maadili, wanatakiwa kujichunga na miiko ambayo hawatakiwi kuivunja.

“Mwaka 2015 hadi Novemba 2016 tumepokea malalamiko 71 kuhusu mawakili, asilimia 45 ya malalamiko hayo yana ukweli,” alisema.

Alisema miongoni mwa malalamiko yaliyowasilishwa ni kutetea wateja chini ya kiwango, kushindwa kutunza siri za wateja.

Jaji Chande aliwataka mawakili kuisaidia mahakama kuondoa mlundikano wa kesi na waziendeshe kwa gharama inayoridhisha.

“Mawakili wanawasilisha maombi na mapingamizi ili kesi ichelewe, kitendo hicho kinawanyima haki watu wengine,” alisema.

Akizungumzia mawakili wapya, Jaji Kiongozi, Ferdinand Wambali, aliwataka washiriki katika kutoa haki, wawe waaminifu kwa mahakama na wateja kwani wakienda kinyume haki itapotea.

Jaji Wambali aliwataka mawakili hao wapya kufika maeneo ya nje ya mji ili wasaidie upatikanaji wa haki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles