25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

POLISI WAVAMIA OFISI YA JAMII FORUMS DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao  huo, Maxence Melo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao huo, Maxence Melo.

Na HERIETH FAUSTINE-DAR ES SALAAM

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam  limevamia ofisi za mtandao wa Jamii Forums (JF) na kufanya upekuzi na kuondoka na vifaa zikiwamo kompyuta kpakato (laptop).

Askari hao walivamia ofisi hizo jana mchana wakiwa wamefuatana  na  na Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao  huo, Maxence Melo, wakafanya  upekuzi na kuwahoji baadhi ya wafanyakazi.

Baada ya kufanya upekuzi ndani ya ofisi hiyo walielekea nyumbani kwa mkurugenzi huyo,  kufanya upekuzi kabla ya kumrudisha  rumande kwa vile hakufikishwa mahakamani.

MTANZANIA lilimtafuta Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam,  Simon Sirro kwa   simu  ili  kupata taarifa kwa kina, lakini haikuweza kupokewa.

Juzi, akizungumza na gazeti hili, mwanaharakati wa kutetea Uhuru wa Mawasiliano, Simon Mkina, alisema Melo alikamatwa na   kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi  ambako aliwekwa selo.

Alisema Melo anakabiliwa na mashtaka ya kuzuia upelelezi wa makosa ya mtandao kwa kushindwa kutoa taarifa binafsi za watumiaji wa mtandao wa Jamii Forums ambazo polisi walizihitaji.

“Max (Melo)alifika  kituoni hapo kuitika wito wa polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, lakini alipofika Kituo Kikuu cha   Polisi  alinyimwa dhamana   kwa madai ya kuwapo amri kutoka   kwa wakubwa,” alisema Mkina akimkariri mmoja wa maofisa wa polisi.

Mkina alisema hata baada ya kuwasiliana na mwanasheria wa Melo, Nakazeel Tenga na kushughulikia dhamana yake, ilishindikana kwa maelezo  kuwa alipaswa kulala kituoni hapo hadi  jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles