22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Rebella atwaa taji la Miss Utalii Kenya

MISS-TOURISM-1VIHIGA, KENYA

MREMBO kutoka Homa Bay, Rebella Omollo, ameshinda tuzo ya Miss Utalii 2016 nchini Kenya katika kinyang’anyiro cha warembo 44 waliotoka maeneo mbalimbali nchini humo.

Rebella aliibuka mshindi usiku wa kuamkia jana huko Vihiga, ukumbi wa Kidudu nchini Kenya.

Shindano hilo lilionekana kuwa na ushindani wa hali ya juu hasa kwa warembo sita waliokuwa wakiwania nafasi tatu za juu lakini Rebella alionekana kufanikiwa kuwashawishi  majaji kutokana na uwezo wake wa kujieleza pamoja na tabasamu lake la kuvutia.

“Tunakubali kwamba hakuna mtu ambaye anakubali kukaa kwenye nchi ambayo haina amani. Kenya ina makabila 42 pamoja na tamaduni 42 lakini wote tunaonekana kuwa pamoja kama Wakenya.

“Tuna amani ya kutosha, hii ni nchi ambayo unaweza ukaishi na wala usione tofauti yoyote. Tunapenda kutumia neno ‘Hakuna matata Kenya’. Tunawakaribisha wageni wote duniani kwa ajili ya kuishi na sisi, kufanya ziara na mambo mengine mengi.

“Napenda kuwashauri Wakenya wenzangu kuipenda nchi yetu kufanya uwekezaji katika biashara, bila sisi wenyewe hakuna atakayekuja kufanya hivyo,” alisema Rebella.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles