27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

RAYVANNY AFUNGA DIMBA KAPO ZILIZOTIKISA 2017

Na CHRISTOPHER MSEKENA

TUKIWA tunaelekea kufunga mwaka 2017, staa wa Bongo Fleva, Rayvanny na mama wa mtoto wake, Fayma wameingia kwenye orodha ya wapenzi wenye umaarufu kwenye tasnia ya burudani zilizoingia kwenye mgogoro.

Wiki hii wawili hao wenye mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Jaydan, wametupiana maneno kwenye mitandao ya kijamii na kuzua gumzo kwa mashabiki ambapo wamekuwa wakiipenda kapo hii ambayo toka mwanzo imeonekana kuwa tulivu kuliko uhusiano wa wasanii wengine wa lebo ya Wasafi.

Mpenzi wa Rayvanny (Fayma) alianza kwa kutangaza kwa mashabiki zake kuwa hivi sasa amekuwa Singo Mama, kisha Rayvanny naye akamjibu kwa kumtakia safari njema huku akimtaka abadilishe jina, kwa kuwa mrembo huyo kwenye mitandao ya kijamii hutumia jina la Fahyvanny, jina alilolichanganya na X wake huyo.

Baada ya hapo, Rayvanny akaweka picha ya mwanawe, Jaydan na kuandika; Miss You Jay Vannyboy, kisha memba mwenzake wa WCB, Harmonize akaandika maneno yaliyothibitisha kuvunjika kwa kapo hiyo, akasema: Bora kuwapenda watoto wetu tu.

Rayvanny, akamjibu Harmonize na kumtaka aache unafiki ambapo Harmonize akarejea tena na kumpa ushauri kwa kusema:  Lakini hapa kaka tusifike huko, mtoto anahitaji matunzo ya baba na mama, tumlaani shetani kwani mwenzio kateleza.

Meneja wa msanii huyo, Babu Tale ambaye yupo naye Marekani  kwa ajili ya kufanya video na msanii Chindoman pamoja na shoo atakayoifanya leo, anasema Rayvanny  amekiri kupishana kauli na mama mtoto wake lakini tayari wameyamaliza.

Mbali na kapo ya Rayvanny, Swaggaz tunakusogezea kapo nyingine za mastaa zilizotikisa mwaka huu ambao unaelekea ukingoni.

 

BARNABA BOY & MAMA STEVE

Mwezi Februari mwaka huu, Barnaba na mama  Steve, (Zuu) waliachana rasmi baada ya mrembo huyo aliyedumu kwenye uhusiano kwa miaka tisa, kuonekana akitoka na msanii chipukizi wa Bongo Fleva anayeitwa Brown.

Wawili hapo bado wanaendelea kuheshimiana na kumtunza mtoto wao, Steve licha ya kuwa hawapo tena kwenye uhusiano.

 

JUX & VANESSA MDEE

Kapo nyingine ni hii ya wanamuziki, Jux na Vanessa Mdee ambao mwaka huu pia wamekuwa gumzo baada ya penzi lao kufahamika kuwa limevunjika.

Aprili 12, mwaka huu kisha kurudi tena Novemva 25, mwaka huu kwenye Tamasha la Fiesta katika mikoa mbalimbali. Chanzo cha wawili hao kugombana hakijafahamika japo kuwa Jux ndiyo mkosaji maana ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kutaka warudiane na ndiye aliyemwomba msamaha Vanessa.

 

NUH MZIWANDA & NAWALI

Agosti 5 mwaka huu, Nuh Mziwanda alitangaza kurudi kwenye dini yake ya awali (Ukristo), akiwa na maana ya kuvunjika kwa ndoa yake ya Kiislamu aliyoifunga na mkewe, Nawal ambaye wamefanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike anayeitwa Anyagile.

Wawili hao walizua gumzo baada ya Nawali kutangaza kumwacha Nuh Mziwanda na kuolewa tena ambapo baadaye ilifahamika kuwa ndoa hiyo ilikuwa bandia na alilazimika kufake, ili aachane na baba wa mtoto wake huyo.

 

HARMONIZE & WOLPER

Mwezi Agosti, mwaka huu, Jacqueline Wolper alitangaza kuachana na Harmonize penzi lililodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja, Harmonize akapata mpenzi mpya mwenye asili ya Italia, anayeitwa Sarah huku Wolper naye akawa na mpenzi wake anayeitwa Brown.

 

DIAMOND & ZARI

Sepetemba 19, mwaka huu, kapo ya Diamond Platnumz na Zari ilitikisa tasnia ya burudani baada ya staa huyo wa muziki kukiri kuchepuka kwenye uhusiano wake na Zari na kuzaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Kapo hii ndiyo imezungumzwa zaidi mwaka huu kutokana na matendo au matukio ambayo yamewakuta pamoja mfano Zari kufiwa na mume wake za zamani, Ivan Don na baadaye kuondokewa na mama yake mzazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles