24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Ratiba VPL yazibana Simba, Yanga

Na Abducado Emmanuel, Dar es Salaam

RATIBA ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu ujao, imeonekana kuzibana timu za Simba na Yanga ambazo zitacheza mechi nyingi ugenini kwenye mzunguko wa pili tofauti na mabingwa watetezi, Azam FC.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo iliyotolewa juzi na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inaonesha Simba na Yanga zitacheza mechi saba nyumbani kwenye mzunguko wa kwanza, huku zikicheza mechi saba ugenini mzunguko wa pili.

Maximo
Kocha mpya wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, Marcio Maximo

Mabingwa watetezi wa taji hilo Azam, wao wana unafuu zaidi kwani kati ya mechi zao 13 za mzunguko wa kwanza ni mechi sita pekee watakazocheza nyumbani, huku mechi saba zilizobakia wakicheza ugenini.

Lakini kwenye mzunguko wa pili, watacheza mechi saba nyumbani na sita ugenini na kuziachia hali ngumu Simba na Yanga, zitakazocheza mechi saba ugenini na sita nyumbani.

Ratiba hiyo inaonyesha Yanga inayonolewa na Mbrazil Marcio Maximo, itaanza mechi yake ya kwanza ugenini kwa kucheza dhidi ya Mtibwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, huku mechi ya mwisho ikimalizia ugenini kwa kucheza na Ndanda FC.

Azam yenyewe itaanzia nyumbani mechi yake ya kwanza kwa kumenyana na Polisi Morogoro iliyopanda daraja, huku ikicheza nyumbani kwenye mechi yake ya mwisho kwa kucheza dhidi ya Mgambo JKT.

Simba iliyoshika nafasi ya nne msimu uliopita wa ligi, itaanzia nyumbani kwenye mechi ya kwanza kwa kukwaruzana na Coastal Union, huku ikimalizia ugenini mechi ya mwisho kwa kupambana na JKT Ruvu.

Ligi hiyo inayotarajia kuanza rasmi Septemba 20 mwaka huu, itasimama kwa siku 26 baada ya mechi ya raundi ya tisa zitakazofanyika Novemba 16 mwaka huu, kupisha michuano ya Kombe la Chalenji na Kombe la Uhai, itaendelea tena Desemba 20 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles