27.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Simba, Yanga kuumana Oktoba 12

Ofisa mtendaji wa bodi ya ligi, Silas Mwakibinga
Ofisa mtendaji wa bodi ya ligi, Silas Mwakibinga

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

WATANI wa jadi Simba na Yanga wamepangwa kukutana kwa mara ya kwanza Oktoba 12, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ratiba hiyo ilionyesha kuwa watani hao watarudiana tena Februari 8 uwanja huo wa Taifa.

Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuanza rasmi Septemba 20, tayari timu hizo zimeshaingia mafichoni kujiweka sawa na ligi hiyo, Simba wakiwa Unguja na Yanga wakiwa Pemba kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa ligi hiyo.

Kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kusainiwa na Ofisa mtendaji wa bodi ya ligi, Silas Mwakibinga, ilionyesha kuwa ratiba nzima ya mechi za ligi zitaanza Septemba 20 kama ilivyopangwa, ambapo Yanga itakutana na Mtibwa Sugar katika mechi ya kwanza Uwanja wa Jamuhuri, huku Simba wakianza na Coastal Union Uwanja wa Taifa.

Mechi nyingine zitakazofungua dimba ni kati ya Azam FC watakao kuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Azam Complex dhidi ya Polisi Morogoro, Stand United ikichuana na Ndanda FC zote zilizopanda daraja msimu huu zikichuana Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Ruvu Shooting itawakaribisha Tanzania Prisons katika Uwanja wa Mabatini Mlandizi, huku Mbeya City wakiwa wenyeji wa nyumbani wa JKT Ruvu Uwanja wa Sokoine.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo imesema mechi zote za Ligi Kuu katika msimu huu, zitakuwa zikichezwa mwishoni mwa wiki ili kuongeza msisimko na kuwapa nafasi mashabiki kuweza kuhudhuria katika kutoa sapoti kwa timu zao, ambapo siku za wiki zimeachwa wazi kwa ajili ya kupisha mechi za Kombe la FA (Federation Cup).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles