31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

Phiri ataka viungo wawe wafungaji

Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri
Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri

NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Phiri ameanza kuwanoa viungo wake ili waanze kufumania nyavu badala ya kuwategemea washambuliaji peke yake.

Katika msimu uliopita, mshambuliaji wa timu hiyo, Amis Tambwe ndiye aliongoza kwa ufungaji, hali ambayo imemlazimu Phiri kutaka na viungo kusaidia timu.

Kiungo wa zamani wa Simba, marehemu Patrick Mafisango, aling’ara kutokana na ujuzi wake wa kufumania nyavu licha ya kuwa kiungo, hivyo kauli ya Phiri huenda inaashiria kuwa na kiungo maridadi kama huyo.

Akizungumza na MTANZANIA, kocha msaidizi wa timu hiyo, Seleman Matola, alisema kwa upande wa safu ya kiungo kocha amewapa mbinu za kuhakikisha wanamiliki mipira, kusaidia na mabeki pamoja na wao kujaribu kufunga kama nafasi inaruhusu na kutoa pasi za haraka.

“Kwa kifupi kocha ameanza kuwanoa upya wachezaji hao kwa lengo la kuhakikisha anatimiza ahadi yake aliyoahidi wakati anaingia nchi ya kunyakua ubingwa msimu huu,” alisema.

Alieleza kocha amekuwa akihakikisha kila mchezaji anazingatia wajibu wake anapokuwa uwanjani, hata mabeki amewataka kujua jinsi ya kukabiliana ipasavyo na timu pinzani.

“Kwa ujumla maandalizi yanaendelea vizuri, kocha amewatoa hofu mashabiki wao kwa kuamini kikosi chao kuwa ndio kitakuwa imara kwa msimu huu wa Ligi Kuu,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles