22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

Ras Inno kuanza kampeni baada ya mfungo

Ras Inno Nganyagwa
Ras Inno Nganyagwa

NA MWANDISHI WETU,

MWANAMUZIKI mkongwe wa muziki wa reggae nchini, Ras Inno Nganyagwa, anatarajia kuzindua kampeni yake ya kurudi upya kwenye ulingo wa muziki baada ya mfungo wa Ramadhani kuisha.

Kampeni hiyo itakayoanzia Iringa mkoa alipozaliwa kwa mwaka jana ilishindikana kutokana na mwingiliano wa uchaguzi mkuu, kutokamilika kwa albamu yake mpya na kutokamilika kwa makubaliano na washiriki wake.

Ras Inno aliliambia MTANZANIA kwamba, kwa sasa ameamua kuwa na kikosi kazi thabiti kinachoweza kutimiza majukumu kwa mujibu wa utaratibu aliojiwekea wa utekelezaji kazi.

“Unajua nilishaacha siku nyingi mfumo wa kufanya kazi kama mtu binafsi ndiyo maana nilisajili taasisi ya kusimamia kazi zangu za muziki ya Reggae Production House Icl ili niweze kutanua wigo wa kutekeleza majukumu katika namna inayofaa zaidi,

“Kwa sasa kikosi changu kipo tayari kuanza kazi ndiyo maana natangaza ujio huu mpya utakaohusisha utambulisho wa toleo la kwanza la albamu yangu mpya ya ‘Love Story’

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles