23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Wasanii wa Barnaba kumsaidia Rais Magufuli

Mulla Flavour na Ice Boy (2)NA CHRISTOPHER MSEKENA,

WASANII wawili kutoka lebo ya ‘Barnaba Boy Classic’ iliyopo chini ya mwanamuziki, Elias Barnabas, kupitia studio yake ya Hightable Sound, Isaya Mwogoti ‘Mulla Flavour’ na Imani Chaula ‘Ice Boy’, wanatoka upya leo na wimbo wao wa pamoja waliouita ‘Tumbua Majipu’.

Mulla, alisema wameamua kutoka na wimbo huo kutokana na juhudi muhimu zinazofanywa na Rais John Magufuli katika dhana yake ya kutumbua majipu watendaji wanaokwenda kinyume na falsafa zake.

“Wasanii wengi wa muziki wa hip hop wamezoea kukosoa hata kama kuna jambo linalostahili pongezi kitu kinachopunguza morali kwa viongozi wetu kutekeleza wajibu wao ndiyo maana uongozi wa Hightable umeamua utoke tofauti.

“Matatizo yapo ila anapotokea kiongozi mkubwa na akaonyesha nia ya kupunguza matatizo tuliyonayo tunapaswa kumpongeza na kumtia moyo zaidi ili aendelee kufanya kazi nzuri. Tumeamua kuwa tofauti na wasanii wengi wa hip hop ambao wamekuwa wakikosoa mambo mengi bila kusifia mazuri,” alisema Mulla.

Naye Ice Boy, aliongeza kuwa wimbo huo umeandaliwa na prodyuza, Emma The Boy chini ya usimamizi wa Barnaba Boy Classic ikiwa ni mwendelezo wa mradi wao wa kuionyesha jamii nchi inakoelekea chini ya Rais Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles