24.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ramos yamemkuta, kutimuliwa PSG

PARIS, Ufaransa

MABOSI wa PSG hawaoni umuhimu wa beki wa kati waliyemtoa Real Madrid, Sergio Ramos, na sasa wanaangalia uwezekano wa kumfungulia mlango wa kutokea.

Kile wanachokiona kuwa ni mzigo, Ramos anayesumbuliwa na majeraha ya kigimbi cha mguu, hajacheza hata mechi moja tangu aliposajiliwa akiwa mchezaji huru na kupewa mkataba mnono wa miaka miwili.

Hata hivyo, mkurugenzi wa michezo wa PSG ni kama amepotezea taarifa hizo akisema wanachofahamu ni kwamba Ramos ni majeruhi, hivyo ataitumikia timu mara tu atakapokuwa fiti.

Endapo PSG watafikia uamuzi wa kusitisha mkataba wake, basi huenda ikawa ni habari njema kwa vigogo wa Ligi Kuu England, Liverpool na Manchester United, kwani zilijaribu kumsajili kabla ya Mhispania huyo kutimkia jijini Paris.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles