25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS WA GHANA ATETEA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI

Accra, Ghana


RAIS wa Ghana, Nana Akufo Addo amewakosoa vikali wapinzani wake na wanaharakati wanaopinga teuzi wake wa mawaziri 110 katika serikali yake mpya.

Rais Addo amesema uamuzi wake wa kuwateua mawaziri 110 ni mkakati wa dharura na mpango wa kuinua uchumi wa nchi hiyo.

Rais huyo wa Ghana alisema uteuzi huo ni miongoni mwa ahadi zake wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika Desemba mwaka jana.

 "Niliahidi kuinua kiwango cha uchumi na kupambana na ufisadi. Hawa mawaziri niliowateua wanakuja kuchapa kazi, hawaji likizo,"alisema Addo.

Wapinzani wa serikali nchini humo hususan katika mitandao ya kijamii wamemshutumu Rais Akufo-Addo kwa hatua yake hiyo ya kuteua baraza kubwa la mawaziri licha ya nchi hiyo kukabiliwa na misukosuko ya uchumi.

George Lawson, Naibu Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress (NDC) amelaani vikali uamuzi huo wa Akufo-Addo na kusema huko ni kuusambaratisha zaidi uchumi wa nchi kwa maslahi ya 'kuwalipa' wapambe wake waliomsaidia katika kampeni za urais.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles