27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

UHABA WA MAJI MOROGORO KUWA HISTORIA

Na ASHURA KAZINJA- MOROGORO


MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka, Mkoa wa Morogoro (MORUWASA), imepokea Dola za Marekani milioni 70 zitakazosaidia kuboresha miradi mbalimbali ya maji mkoani hapa.

Akizungumza kwenye wiki ya maji iliyowashirikisha madiwani na watendaji wa kata, Mkurugenzi wa MORUWASA, Nicholaus Angumbwike, alisema fedha hizo zilizotolewa na shirika la misaada la Ufaransa tayari zimeshaanza kutumika katika uchimbaji wa visima vitano ili kupunguza uhaba wa maji kutokana na ukame uliojitokeza.

Angumbwike alisema visima hivyo vitachimbwa katika maeneo ya Lita, Kola, Bigwa Sokoni, Lukobe na Tenki la Tumbaku.

“Fedha hizo zinatarajia kuingizwa katika mradi mkubwa wa kuondoa udongo katika Bwawa la Mindu ili kuliongeza kina kwa mita 2.5, baada ya bwawa hilo kujaa mchanga na kupoteza kina chake halisi cha uhifadhi wa maji.

“Pia, utajengwa mtambo mpya wa kusafisha maji katika kituo cha kusafisha maji cha mafiga kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha maji lita 270 kwa saa ili kufanya ongezeko la maji kwa wakazi wa Mkoa wa Morogoro. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwaka 2020,” alisema Angumbwike.

Pamoja na hayo, aliwaomba madiwani watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa juu ya watu wanaoiba maji katika kata zao.

Naye Diwani wa Kata ya Sabasaba, Mudhihiri Shoo, aliishauri mamlaka hiyo kujenga utaratibu wa kuchimba mabwawa ya kutosha kuhifadhi maji ili kuufanya Mkoa wa Morogoro, usikumbwe na uhaba wa maji.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Mwembesongo, Rashidi Kalumbwana, aliiomba MORUWASA kuhakikisha wananchi hawakosi maji kwa kipindi chote cha uondoaji wa tope katika Bwawa la Mindu, ili kuepusha usumbufu kwa wananchi wanaotegemea maji kutoka MORUWASA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles