25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

VIJANA MAREKANI WAENDELEA KUMPINGATRUMP

Newyork -Marekani


UTAFITI uliofanywa na Shirika la GenForward inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya vijana wa Marekani wanamtazama Donald Trump kama rais ambaye si halali, mpuuzi na asiyekuwa na sifa za uongozi. Utafiti uliochapishwa na Shirika la Habari la AP juzi unaonesha kuwa asilimia 57 ya vijana nchini Marekani wanahisi kuwa Trump ni 'rais haramu na asiyefaa'.

Utafiti huo umebainisha kuwa, asilimia 75 ya vijana wa Marekani wenye asili ya Afrika na asilimia 50 ya vijana weupe wa Kimarekani wanahisi kuwa Trump ni rais asiyejiheshimu.

Kwa mujibu wa utafiti huo wa GenForward, vijana wanane kati ya kumi nchini Marekani hawakubaliani na sera za Trump na mfumo wake wa uongozi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles