BANJUL, GAMBIA
RAIS wa Gambia, Yahya Jammeh, atakuwa kiongozi wa waasi iwapo atashindwa kuondoka madarakani mwishoni mwa muda wake wa uongozi Januari mwakani.
Msemaji wa muungano wa upinzani ambao ulimuingiza madarakani Rais mteule Adama Barrow, amesema kiongozi huyo wa muda mrefu hana mamlaka ya kikatiba kubakia madarakani baada ya Januari.
Jammeh awali alikubali kushindwa baada ya miaka 22 madarakani, lakini siku chache baadaye alibatilisha matokeo ya uchaguzi akitaka urudiwe upya.