30 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

MUSYOKA AELEZA WALIVYOPINGA CHAGUO LA MOI URAIS 2002

NAIROBI, KENYA


kalonzo-musyoka KIONGOZI wa Chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, ametoa kitabu cha maisha yake, pamoja na mambo mengine akieleza namna walivyokiasi kilichokuwa chama tawala tangu uhuru, Kanu.

Anaeleza kuwa uasi huo ulikuja baada ya juhudi za Rais mstaafu Daniel arap Moi za kuleta maridhiano kati ya waasi wa chama cha Kanu na Rais Uhuru Kenyatta aliyemteua kugombea urais kupitia chama hicho mwaka 2002 kugonga mwamba.

Katika kitabu hicho, ‘Against All Odds’ (Dhidi ya Vikwazo Vyote), kilichoandikwa na mwandishi Caleb Atemi, kinachotarajiwa kuzinduliwa kesho, Musyoka anaeleza uwapo wa mlolongo wa mikutano Ikulu, kabla ya uchaguzi mkuu wa 2002.

Chama cha Kanu kilishindwa vibaya na muungano wa NARC kwenye uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa Musyoka, mkutano uliofanyika Oktoba 10, 2002 ulihudhuriwa na kinara wa Cord, Raila Odinga, marehemu Prof George Saitoti, Moody Awori, Nicholas Biwott na Yusuf Haji, walimkabili Moi na kumwambia kuwa Kanu ingeshindwa vibaya uchaguzi huo ikiwa hatabadili uamuzi wake.

Hata hivyo, Moi aliwajibu kwamba walikuwa wakimpinga yeye, si uamuzi wake wa kumteua Uhuru.

“Hampingi chaguo langu (Uhuru) ila mimi,” alisema.

Hata hivyo, Musyoka alimjibu Moi: “Ikiwa ni hivyo (Mzee) nakuomba kwa heshima na kwa niaba yetu sote pamoja na chama kujiondoa katika mchakato huu. Itakuwa bora kuwashirikisha wajumbe wa chama kumchagua atakayewania urais katika Uwanja wa Michezo wa Kasarani.”

Hata hivyo, kauli hiyo iliashiria mwisho wa mkutano huo, uliofanyika wakati KANU ikijitayarisha kwa kongamano la wajumbe na Uhuru alipitishwa kuwania urais.

Musyoka alisema kuwa huo ndio ulikuwa mkutano wa mwisho kati yao na Moi.

Kutoka hapo, viongozi waasi walifahamu hawapo tena katika chama hicho.

“Walikuwa wameanza kubadilisha majina ya wajumbe, hata wilaya tunazotaka. Tulijua kwamba walikuwa wakijitayarisha kutufurusha chamani,” alisema.

Baada ya mkutano huo wa Ikulu, viongozi waasi walielekea katika Mkahawa wa Serena ambako waliwahutubia wanahabari kuhusu msimamo wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles