23.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Ufilipino kuacha siasa

RAIS wa Ufilipino, Rodrigo Duterte, ametangaza kuwa si tu hatagombea nafasi ya makamu wa rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani, pia amepanga kuachana na siasa.

Duterte aliingia madarani mwaka 2016 na umaarufu wake mkubwa hata nje ya Ufilipino umetokana na kile kinachotajwa kuwa ni utawala wake kutekeleza mauaji dhidi ya wahalifu, hasa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Mwezi uliopita, kiongozi huyo alisema angegombea nafasi hiyo ya makamu wa rais, ikifahamika kuwa hawezi kuiwania ile ya urais kwa kuwa Katiba inazuia kukaa Ikulu kwa zaidi ya mihula miwili aliyotumikia.

Kwa upande mwingine, zipo taarifa zinazonyetisha kuwa binti yake, Sara Duterte-Carpio, anajiandaa kugombea kiti cha urais akiamini katika uzoefu wake wa kuwa Meya wa Jiji la Davao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles