MWANAUME raia wa Lithuania amefanyiwa upasuaji na kukutwa na kilogramu zaidi ya moja ya misumari, nati na visu kwenye tumbo lake.
Upasuaji huo uliochukua saa tatu ulifanyika katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Klaipeda na madaktari wamekiri kuwa hilo ni jambo la ajabu zaidi kuwahi kukutana nalo katika shughuli zao.
Kwa mujibu wa kile kilichoelezwa na madaktari, mwanaume huyo alifikishwa hospitali kwa gari la wagonjwa na kilichokuwa kikimsumbua ni maumivu makali ya tumbo.
Wakizungumzia sababu ya vifaa hivyo kukutwa mwilini, madaktari wamesema jamaa alikuwa akimeza kimoja kimoja kila siku, akifanya hivyo ndani ya mwezi mmoja ili tu asahau tabia yake ya kunywa pombe.Juu ya hali yake, jamaa anaendelea vizuri, ingawa bado madaktari wa Hospitali hiyo wanaendelea kuifuatilia hali yake