29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Trump kigeugeu, aitetea Saudi Arabia

WASHINGTON, MAREKANI

SIKU chache tu baada ya kutishia kuiwekea Saudi Arabia vikwazo kutokana na madai ya kumuua mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi, Rais wa Marekani Donald Trump sasa ameikingia kifua nchi hiyo.

Rais Trump badala yake amesema si vyema kuihukumu Saudia bali kuwa na subira hadi uchunguzi kuhus suala hilo utakapokamilika.

Kwenye mahojiano na Shirika la Habari la Associated Press, Trump amekifananisha kisa cha Khashoggi ambaye maafisa wa Uturuki wanasema aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul, na madai ya udhalilishaji wa kingono dhidi ya Jaji wa Mahakama ya Juu wa Marekani Brett Kavanaugh.

Trump amesema, “nafikiri tunastahili kujua kilichotokea kwanza. Hapa tena, ni kile kisa cha mtu kuwa na hatia mpaka atakapothibitishwa ni msafi. Tumeshuhudia kitu kama hiki katika suala la Jaji Kavanaugh na hana hatia siku zote kulingana na mimi,” mwisho wa kunukuu.

Kauli hii ya Trump. ndiyo ya wazi kabisa ambapo anaonesha kuitetea Saudi Arabia, nchi ambayo ameifanya kuwa kituo chake kikuu cha kutimiza ajenda zake Mashariki ya Kati.

Wakati huo huo, gazeti linaloiunga mkono Serikali ya Uturuki limechapisha taarifa namna Khashoggi alivyouawa katika ubalozi huo, wakati ambao Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo yu Uturuki kwa mazungumzo na Rais Reccep Tayyip Erdogan kuhusu suala hilo.

Pompeo amewasili Uturuki akitokea Saudia na amesema katika mazungumzo yake na viongozi wa Saudi Arabia  wamekubaliana chunguzi kuhusiana na suala hilo utakuwa wazi.

“Walisema wazi watauonyesha ulimwengu mzima matokeo ya uchunguzi wao. Walisema pia watamaliza uchunguzi huo kwa haraka. Sijui ni lini lakini walisema wanaelewa umuhimu wa kumaliza haraka ili waweze kujibu maswali muhimu,”

Huku Pompeo akitazamiwa kufanya mazungumzo huko Uturuki, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa nchi hiyo amesema polisi waliokuwa wakichunguza ubalozi mdogo wa Saudi Arabia Istanbul walipata ushahidi kuwa Khashoggi aliuawa katika ubalozi huo.

Uturuki kupitia kwa Waziri wa Usalama wa Ndani, Suleyman Soylu imesema inasubiri makubaliano ya pamoja na Saudi Arabia kufanya uchunguzi katika makao ya balozi wa Saudia mjini Istanbul.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles