22.2 C
Dar es Salaam
Friday, July 5, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia, Nyusi kufungua rasmi Maonyesho ya Sabasaba, Msumbiji ni kati ya Nchi Shiriki

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa kesho yeye pamoja na mwenyeji wake, Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji, watakuwa katika viwanja vya Sabasaba kwa ajili ya ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Sabasaba.

“Eneo jingine tulilozungumzia ni kama mnavyojua kesho Mheshimiwa Rais na mimi mwenyeji wake tutakuwa viwanja vya Sabasaba na atafanya ufunguzi rasmi wa maonyesho ya Sabasaba,” alisema Rais Samia.

Rais Samia alibainisha kuwa Msumbiji ni moja ya nchi za Kiafrika ambazo zimeshiriki katika maonyesho hayo. Rais Nyusi ataeleza aina ya ushiriki wa Msumbiji katika maonyesho hayo.

“Na katika nchi za Kiafrika ambazo zimeshiriki, Msumbiji ni moja ya nchi ambazo zimeshiriki na mwenyewe ataeleza wamekuja kwa ushiriki wa aina gani,” aliongeza Rais Samia.

Rais Samia alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Nyusi na kusisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao pamoja na nchi nyingine za Afrika.

“Kwa hiyo nataka nimshukuru sana Mheshimiwa Rais, lakini hili tumekubaliana kuongeza ushirikiano haswa wa kuunganisha nchi zetu na nchi za Afrika,” alisema Rais Samia.

Ufunguzi huu rasmi wa maonyesho ya Sabasaba unatarajiwa kuwa ishara ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na kijamii kati ya Tanzania, Msumbiji, na nchi nyingine za Afrika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles