28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Tanzania na Msumbiji kuanzisha Kituo kimoja cha Forodha Mtambaswala ili kukuza Biashara

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametangaza mpango wa kuanzisha kituo kimoja cha forodha katika eneo la Mtambaswala, Tanzania, na upande wa pili nchini Msumbiji. Hatua hii inalenga kuhamasisha na kurahisisha biashara kati ya nchi hizo mbili.

“Tumekubaliana kuanzisha sasa kituo kimoja cha forodha kule Mtambaswala kwetu sisi Tanzania na upande wa pili Mozambique kuwe na kituo kimoja kitakachohamasisha biashara,” alisema Rais Samia.

Rais Samia alieleza kuwa biashara kati ya Tanzania na Msumbiji ilifikia Dola Milioni 57.8 mwaka 2022. Hata hivyo, biashara hiyo ilipungua mwaka 2023, na nchi hizo mbili zimekubaliana kuchunguza sababu za kuporomoka kwa biashara hiyo.

“Biashara ya Tanzania na Mozambique ilikuwa Dola Milioni 57.8 mwaka juzi 2022. Lakini mwaka jana tumeshuka. Kwa hiyo tumekubaliana kuangalia sababu gani,” alisema Rais Samia. “Labda usalama ulizorota, baadhi ya mipaka vile vichochoro wanavyopita wafanyabiashara tulifunga.”

Rais Samia pia alibainisha kuwa inawezekana baadhi ya miamala haifanyiki rasmi kutokana na urefu wa mpaka kati ya nchi hizo mbili, ambapo wafanyabiashara wanaweza kupenya na kufanya biashara zao nje ya takwimu rasmi za serikali.

“Inawezekana pia baadhi ya miamala hazipatikani rasmi. Kama mnavyojua mpaka wetu ni mrefu. Kwa hiyo wafanyabiashara wanapenya penya na zile takwimu zinatupita,” alieleza Rais Samia.

Mpango wa kuanzisha kituo kimoja cha forodha unatarajiwa kuimarisha usalama na kuwezesha urahisi wa biashara rasmi, hivyo kuongeza takwimu za biashara na kuboresha uchumi wa nchi hizo mbili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles