28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia: Tanzania na Msumbiji Kuunda Umoja wa Wazalishaji wa Korosho Afrika

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ametangaza kuwa Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kuunda umoja wa wazalishaji wa korosho Afrika, ili kuwa na sauti moja katika masoko ya kimataifa.

“Katika upande wa kilimo, Msumbiji na Tanzania sote ni wazalishaji wa korosho. Tunazalisha korosho za kutosha. Lakini kama mnavyojua kwamba sisi si wapangaji wa bei ya korosho duniani. Tunajaribu kupanga bei za korosho hapa ndani,” amesema Rais Samia.

Rais Samia alifafanua kuwa moja ya mikakati ni kuhakikisha kuwa wale wanaonunua korosho ndani ya nchi wanapata bei nzuri, hivyo kuchochea uzalishaji na kuongeza kipato kwa wakulima.

“Ndio maana tunakwenda njia tofauti ambazo zinawafanya watu wanaonunua korosho ndani angalau basi inone kidogo,” alieleza Rais Samia.

Katika juhudi za kuimarisha ushirikiano huu, Rais Samia alisema walikubaliana kuunda umoja wa wazalishaji wa korosho Afrika. Aliendelea kueleza kuwa Rais wa Guinea-Bissau, Umaro Sissoco Embaló, alikubali wazo hili alipolitembelea Tanzania.

“Tumekubaliana kuunda umoja, na mnakumbuka alipokuja Rais wa Guinea Bissau, Mheshimiwa Embaló, nilimuuzia wazo hili naye amekubaliana. Kwa hiyo, kwa pamoja sasa wazalishaji wa korosho Afrika tutakwenda kufanya umoja wetu ili tuwe na sauti moja katika masoko,” amesema Rais Samia.

Umoja huu unatarajiwa kusaidia nchi za Afrika zinazozalisha korosho kuwa na ushawishi zaidi katika masoko ya kimataifa, na hivyo kuboresha bei na faida kwa wakulima wa korosho katika bara hili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles