26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Samia ayafunda mashirika yasiyo ya kiserikali

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Rais Samia Suluhu Hassan ameyataka mashirika yasiyo ya kiserikali kuzingatia mipango na vipaumbele vya Kitaifa katika kutekeleza majukumu na miradi mbalimbali ya maendeleo.

Rais Samia amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika mkutano wa mwaka wa mashirika hayo.

“Napenda kuyaelekeza mashirika yasiyo ya kiserikali kuwa na mpango mkakati wa maendeleo utakaokwenda sambamba mpango wa Taifa wa miaka mitano,” amesema.

Ameongeza kuwa huko nyuma mashirika mengine yalikuwa yakifanya kazi kulingana na matukio ukianzishwa mpango mazingira yanakimbilia huko ili kushawishi fedha za wafadhili.

“Ni imani yangu mtajipanga upya kufanya kazi kwa ufanisi, kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu na miradi mbalimbali kwa kuzingatia tamaduni, mila na desturi za nchi,” amesema Rais.

Rais Samia akizindua taarifa ya mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali  wakati wa mkutano wa mwaka jijini Dodoma

Rais Samia ameyataka mashirika ya ndani kupunguza utegemezi kwa wafadhili na wadau wa maendeleo kutokana na mabadiliko ya Sera na Agenda za wadau hao bali waanzishe miradi ya kuwatengenezea fedha kwa kushirikiana na Serikali. 

Aidha ameyataka mashirika hayo  kuhamasisha zoezi la sensa likatalofanyika nchini mwaka 2022 ili Taifa liweze kujiletea maendeleo katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dorothy Gwajima amempongeza rais kwa uongozi wake mahiri uliowezesha mashirika hayo kupata uongozi na kufanya kazi katika mazingira mazuri.

Ameongeza kupitia mkutano huo mashirika hayo yamepata semina elekezi kuhusu sheria, kanuni na miongozo hivyo ni matumaini kuwa wamefahamu wanatakiwa kufanya nini.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Dk. Lilian Badi amesema watazingatia sheria, kanuni na miongozo pamoja na kushirikiana na serikali ili kutoa mchango wenye tija nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles