23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Nkurunziza aishtaki televisheni ya Ufaransa

PARIS, UFARANSA

MAHAKAMA nchini Ufaransa imeanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza dhidi Televisheni moja ya nchini Ufaransa, Mwanasheria wa Ubelgiji na Mwandishi wa Habari wa Burundi, David Gakunzi, kwa makosa ya kuikashifu nchi yake na hadhi yake.

Rais Nkurunziza anadai kuwa Televisheni hiyo ya Ufaransa miaka miwili iliyopita ilionyesha picha za video za mauaji ya kimbari kwa madai kuwa chama tawala cha Burundi ndicho kilichohusika.

Aidha, amesema kuwa picha hizo za video zilizoonyeshwa na televisheni ya Ufaransa, Channel 3, zinadai mauaji hayo ya watu wengi yalifanyika katika viunga vya makazi ya Rais Nkurunziza, jambo linalokanushwa na ambalo kwa sasa limefikishwa mahakamani.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili ya BBC, Rais Nkurunziza amekanusha vikali kwamba picha hizo wala si za ndani ya Burundi, bali zinavyoonekana ni kama zilichukuliwa mahali fulani katika nchi za Afrika Magharibi.

Televisheni hiyo ya Channel -3 ya Ufaransa ilizirusha picha hizo mwaka 2016, wakati wa uchaguzi mkuu wa Burundi, ulioandamana na vurugu.

Video hizo katika matangazo kupitia televisheni ya France Channel 3, zilionyesha mauaji ya watu wengi, yanayodaiwa kutekelezwa na wafuasi wa Rais Pierre Nkurunziza.

Picha hizo za video zimepewa jina la ‘Proof of acts of violence in Burundi”, ikimaanisha ‘Ushahidi wa vitendo vya machafuko ya Burundi.”

Ndani ya picha hizo pia baadhi ya watu wanaonekana wakizungumza lugha ya Kihausa, lugha ambayo haiongelewi nchini Burundi.

Mshitakiwa Bernard Maingai, ambaye ni mwanasheria, anatuhumiwa kwamba ndiye aliyepeleka video hiyo ili ichezwe katika runinga, wakati mwandishi wa habari, David Gakunzi, yeye anashitakiwa na Rais Nkurunziza kwa tuhuma za mahojiano aliyoyafanya kwenye runinga, akizungumzia picha hizo.

Serikali ya Burundi imekuwa ikipata vikwazo kutoka kwa jumuiya za kimataifa, kwa madai ya kukiuka haki za binadamu na kwamba chama tawala nchini humo kina kundi la vijana linaloitwa Imbonerakure. Hata hivyo, Serikali ya Burundi imekuwa ikipinga madai hayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles