28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Mwinyi: Maonyesho ya Sabasaba yamedhihirisha utayari wa kufungua milango ya mataifa 22

Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Husein Ali Mwinyi, amesema Maonyesho ya 46 ya Sabasaba yamedhihirisha utayari wa kufungua milango ya mataifa 22 kushirikiana na kampuni za ndani ili kuongeza ushindani kati ya bidhaa za ndani na nje.

Rais Dk.Mwinyi almeyasema hayo jijini Dar es Salaam baada ya kutembelea Maonyesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba).

“Maonyesho yanafanyika kila mwaka na ninakuja lakini ya mwaka huu ni tofauti, Tanzania tumepiga hatua na tupo katika njia sahihi ya kufikia maendeleo,”amesema Dk. Mwinyi.

Ameongeza kuwa mabadiliko hayo yameonekana hata kwa wafanyabiashara wadogo, ambapo wamezingatia ubora wa bidhaa na vifungashio.

“Utayari wa Tanzania ni mkubwa katika kuvutia wawekezaji, serikali zote mbili zipo tayari kwa ajili ya sekta hiyo na biashara,”amesema Dk. Mwinyi. 

Kwa upande wake Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji, amesema atahakikisha wanatumia maonyesho hayo kukuza sekta ya teknolojia ili kuimarisha ufanyaji biashara wa kisasa na uwekezaji wenye tija.

“Utayari wa taasisi zitakazoshiriki kliniki ya biashara na taasisi za serikali zinazotoa huduma na kufanyia kazi changamoto zilizopo katika maonyesho haya ni muhimu ili kufikia maendeleo tunayoyataka,”alisema.

Alitumia fursa hiyo, kuwataka wanawake kuwa tayari kwa ajili ya kongamano kubwa la wafanyabiashara wanawake Afrika litakalofanyika mwezi ujao nchini.

“Rais Samia Suluhu Hassan amenitaka nihakikishe nawajengea uwezo wafanyabiashara wanawake na kuwaonyesha njia katika biashara ili kufikia fursa za ushindani wa soko la Afrika, nimemuahidi natoa wito kwa wanawake wenzangu tuitumie nafasi hiyo,” amesema Dk. Kijaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles