22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 14, 2024

Contact us: [email protected]

PSSSF yawataka wanachama wake kujisajili kidigital Sabasaba

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

MFUKO wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), umewataka wanachama wake kutembelea katika banda lao lililopo katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 46 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere ili kuhakikiwa taarifa zao kwa mfumo wa alama za vidole.

Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho hayo, Meneja uhusiano wa PSSSF, James Mlowe amesema lengo la kuanzisha mfumo huo ni kupunguza mludikano wa Wanachama wao ambao wamekuwa wakifika katika ofisi zao.

Alisema kisheria kila mwaka wamekuwa wakifanya zoezi la kuhakiki Wana achama wao kwa njia ya kawaida.

“Kwa sasa tumeanzisha mfumo wa alama za vidole ambao umelenga kumsaidia mwanachama kutunza kumbukumbu zake vizuri na pia ataweza kutumia mfumo huu popote pale alipo,” amesema Mlowe.

Amesema huduma hiyo ya PSSSF kiganjani na PSSSF mtandaoni huduma hizo ni suluhisho la kuokoa muda kwa wanachama wastaafu pamoja na waajiri.

Mlowe amesema PSSSF imetenga Sh billioni 60 kwa wastafu zaidi ya160,000 ambazo uzitoa kwa kila mwezi kwa ajili ya kujikimu kiuchumi.

Aidha, amesema wanachama watakaotembelea banda lao watapata fursa ya kupata elimu kuhusu mfuko.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles