Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Liberata Mulamula amefanikiwa kutembelea Banda la Watumishi Housing Investments lililopo katika viwanja vya sabasaba ndani ya ukumbi wa Karume na kupatiwa maelezo ya kina juu ya upatikanaji wa Nyumba Bora kwa Bei nafuu kwa watumishi wa umma, wafanyakazi wa sekta binafsi, wafanyabiashara na wanachama wote wa mifuko ya hifadhi ya jamii.Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Investments (WHI), Dk. Fred Msemwa, akisikiliza na kuhudumia wateja wanaoendelea kutembelea banda letu katika maonesho ya 46 ya sabasaba. Banda ka WHI lipo katika banda kubwa la Karume. Mtanzania unakaribisha kutembelea banda hilo kwa ajili ya kujipatia nyumba kwa bei nafuu.