Na MWANDISHI WETU
Rais wa Dk. John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi watatu leo Novemba 24, akiwamo Rais mstaafu wa Zanzibar.
Rais Magufuli amemteua Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Dk. Shein anachukua nafasi ya Jaji mstaafu Barnabas Samatta ambaye anamaliza muda wake.
Rais Magufuli pia amemteua, aliyekuwa mbunge wa Kyera na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo mstaafu, Dk. Harrison Mwakyembe kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
“Dk. Mwakyembe anachukua nafasi ya, Mariam Mwaffisi ambaye amemaliza muda wake,” imeeleza taarifa hiyo.
Aidha, Rais Magufuli amemteua, Gaudencia Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
“Gaudensia Kabaka anashika wadhifa huo kwa kipiudi cha pili baada ya kipindi cha kwanza kumalizika,” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza leo Novemba 24, 2020.
ReplyForwa |