26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Kimei akabidhi mchango wa mabweni

Na MWANDISHI WETU-MOSHI

IKIWA ni takribani mwezi mmoja tangu kuchaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu, aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei ameanza utekelezaji wa ahadi zake kwa kasi kubwa.

Jana, Dk Kimei alikabidhi Sh milioni nne ambayo ni ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni kuunga mkono ujenzi wa mabweni ya wasichana kwa Shule ya Sekondari Ghona iliyopo katika Kata ya Kahe Mashariki.

“Nawahakikishia ahadi tulizozitoa wakati wa kampeni pamoja na zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa kushirikiana na Serikali, wadau wa maendeleo pamoja na ninyi wananchi tutazitekeleza.

“Katika kuwathibitishia hilo leo nimefika kukabidhi Sh milioni nne ambayo niliahidi wakati wa kampeni kuwaunga mkono ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule hii.

“Nitaendelea kushirikiana nanyi kwa kuendelea kuchangia na kutafuta wadau wengine pia watuunge mkono ili tufanikishe ujenzi huu kwa haraka na kuwapa mabinti zetu mazingira mazuri ya kusoma. Nawaomba ushirikiano ili tuijenge Vunjo yetu kwa kasi,” alisema Dk. Kimei.

Bweni hilo la wasichana katika shule hiyo linagharama ya zaidi ya milioni 120 na wadau wa maendeleo wanaendeela na juhudi za kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kupitia njia mbalimbali.

Akizungumza, Diwani wa Kata hiyo ya Kahe Kulwa Kamili Mmbando, alisema anamshukuru mbunge kwa hatua hiyo aliyofikia.

Mkuu wa Shule iiyopewa mchango huo, Elly Maro alisema shule hiyo imekuwa na changamoto za bweni na wanafunzi wamekuwa wanatoka mbali jambo ambalo linafanya baadhi ya wanafunzi kufika shuleni saa tano mchana ila kwa sasa baada ya bweni litakapokamilika litapunguza changamoto hiyo.

Katika hafla hiyo, walihudhuria Diwani wa Kata hiyo, Kulwa Kamili Mmbando, wajumbe wa bodi ya shule, walimu, wenyeviti wa
vijiji Kata ya Kahe Mashariki na wajumbe wa kamati ya siasa CCM kata ya Kahe Mashariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles