27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Magufuli aagiza mamilioni ya sherehe ya Bunge yapelekwe Muhimbili

John-MagufuliNa Mwandishi Wetu

RAIS John Magufuli ameagiza zaidi ya Sh milioni 200 zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla ya uzinduzi wa Bunge la 11 zipelekwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya kwenda kununulia vitanda vya wagonjwa.

Akizungumza katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bunge la 11 iliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Rais Magufuli alisema ni jambo jema kwa wabunge kujinyima ili kuwasaidia wagonjwa walioko Muhimbili.

“Nilipoambiwa zimechangwa Sh milioni 225 kwa ajili ya sherehe, nikasema fedha hizo zipelekwe katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda.

“Kwa kufanya hivyo tutakua tumejinyima sisi wenyewe lakini tutakuwa tumewanufaisha wenzetu ambao wana matatizo makubwa yanayoweza kutatuliwa kwa fedha hizo,” alisema Rais Magufuli.

 

Awali akitoa taarifa ya michango hiyo, Ofisa wa Bunge, Said Yakubu, alisema jumla michango iliyopatikana kwa ajili ya kuandaa tafrija hiyo ni Sh milioni 225 lakini zilizotumika ni Sh milioni 24 tu baada ya kuzingatia maagizo ya Rais Magufuli.

Aliwataja wadau waliochangia fedha kwa ajili ya sherehe hiyo kuwa ni Benki ya Makabwela (NMB), CRDB, Benki ya Afrika, PSPF na PPF.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles