27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

RAIS MADURO ATUHUMIWA KUPOKEA RUSHWA

BRAZIL

MWENDESHA mashitaka wa zamani wa Venezuela Luisa Ortega Diaz jana amefichua kuwa na ushahidi unaomhusisha Rais Nicolas Maduro na kundi la maofisa wengine kupokea hongo kutoka kampuni moja ya ujenzi.

Hilo limekuja wiki chache tu tangu wafuasi wa upinzani wafanye mgomo na maandamano ya kupinga utawala wake.

Aidha Maduro anatuhumiwa kutaka kubadili Katiba, suala ambalo pia liliingiliwa na Rais wa Marekani Donald Trump akionya nia ya Maduro huenda ikaathiri uchumi wa taifa hilo.

Akihutubia wanahabari mjini Brasilia, Brazil, Diaz amewataja wanaotuhumiwa kuchukua hongo ni pamoja na Rais Maduro.

“Makamu Rais wa chama tawala, Diosdado Cabello na Jorge Rodriguez, ni miongoni mwa waliochukua hongo pamoja na Rais Maduro,” amedai Diaz.

Hata hivyo, kwenye kikao tofauti, mwendesha mashtaka mpya Tarek Saab ambaye anatuhumiwa pia na Diaz anasema kuwa madai hayo hayana ushahidi.

“Tetesi za Diaz hazina ushahidi wowote,” amedokeza Tarek akiongea mjini Caracas.

“Diaz alifukuzwa serikalini kwa kwenda kinyume na maadili. Miaka 10 akiwa kazini alishindwa kuchunguza tuhuma za rushwa,” ameongeza.

 

Rais wa Marekani Mike Pence amesema kuwa utawala wa Rais Trump unatarajia kuongeza nguvu kwa Venezuela ili kurejesha utawala wa kidemokrasia.

“Kuanguka kwa nchi ya Venezuela kuna madhara kwa ukanda mzima na kusababisha ongezeko la usafirishaji wa dawa za kulevya na ongezeko la wahamiaji kinyume cha sheria,” alisema Pence.

Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles