31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

BEKA AKANUSHA BIFU LAKE NA ASLAY

Na JOHNS NJOZI-DAR ES SALAAM

MSANII wa Bongo Fleva, Bakari Katuti ‘Beka’, amekanusha kuwa kwenye ugomvi na msanii mwenzake, Aslay Isihaka ‘Aslay’.

Awali Beka na Aslay walikuwa wakifanya muziki pamoja katika kundi la Yamoto band, huku wakisaidiana na wasanii wengine ambao ni Enock Bella na Maromboso.

Akizungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu jana, Beka alisema hata kazi zake ambazo amekuwa akizifanya hazina ushindani wowote na Aslay.

“Mimi na Aslay hatuna ugomvi wala tatizo, sijawahi kutoa wimbo kwa ajili ya kushindana naye, kwani kila mtu anafanya kazi kivyake,” alisema Beka.

Alisema mipango yake si kutoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja, bali ni kujipanga na kuhakikisha anafanya kazi nzuri itakayoweza kudumu kwa muda mrefu masikioni mwa mashabiki wa muziki wake.

Beka alisema mbali na kufanya kazi zake binafsi, pia bendi yao ya Yamoto itaendelea kuwepo na muda mwafaka utakapofika watasikika tena.

“Yamoto tutarudia mafanikio ya kujitegemea na kufanya kazi binafsi, hayawezi kututenganisha sisi si wasanii wa kwanza kufanya hivi,” alisema Beka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles