25.5 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

RAIS BASHAR AL-ASSAD ARUDISHA TUZO UFARANSA

DAMASCUS, SYRIA


SERIKALI ya Syria imerejesha Ufaransa tuzo ya Légion d’honneur aliyopewa Rais Bashar al-Assad, ikisema kuwa haiwezi kuchukua tuzo kutoka taifa ambalo limekuwa ‘mtumwa’ wa Marekani.

Hatua hiyo inajiri siku moja tu baada ya Ufaransa kusema taratibu za kinidhamu za kuifuta tuzo hiyo zinakaribia kukamilika.

Miongoni mwa viongozi waliopewa tuzo hiyo ni pamoja na aliyekuwa Rais wa Tunisia, Zine El Abiine Ben Ali mwaka 1989 na mshirika wa Assad, Rais wa Urusi Vladimir Putin mwaka 2006.

Hadi sasa ni rais mmoja tu aliyepokonywa tuzo hiyo, Rais wa zamani wa Panama Manuel Norriega.

Aidha hivi majuzi nyota wa Hollywood Harvey Weinstein alipokonywa tuzo hiyo baada ya kukabiliwa na mashtaka ya unyanyasaji wa kingono.

Ufaransa hivi karibuni ilijiunga na Marekani na Uingreza kuishambulia Syria kufuatia madai ya kutumia silaha za nyuklia dhidi ya raia wake.

Tuzo hiyo ilirudishwa Ufaransa kupitia ubalozi wa Italia mjini Damascus.

Rais Assad alipewa tuzo hiyo ya hadhi ya juu mwaka 2001 baada ya kuchukua madaraka kufuatia kifo cha baba yake.

”Wizara ya Mambo ya Nje imerudisha Jamhuri ya Ufaransa tuzo ya Légion d’honneuri aliyopewa Rais Assad”, wizara hiyo ilisema katika taarifa yake juzi.

“Si heshima kwa Rais Assad kuvaa tuzo iliyotolewa na taifa mtumwa na mfuasi wa Marekani anayeunga mkono ugaidi”, iliongoza.

Takriban watu 3,000 kila mwaka hutuzwa tuzo hiyo ya hadhi ya juu kwa huduma waliyotoa kwa Ufaransa au kutetea haki za binadamu, uhuru wa kujieleza ama sababu kama hizo.

Marekani, Uingereza na Ufaransa zilishambulia maeneo kadhaa ya Serikali ya Syria Jumamosi wiki mbili zilizopita ili kujibu matumizi ya silaha za kemikali katika mji wa Douma.

Jeshi la Syria lilituhumiwa kutumia silaha hizo za sumu dhidi ya raia wa mji huo uliokuwa wa mwisho kukaliwa na waasi katika jimbo la mashariki mwa Ghouta nje ya Damascus.

Zaidi ya watu 40 walifariki dunia katika shambulio hilo la Aprili 7, kwa mujibu wa wanaharakati wa upinzani, wafanyakazi wa uokoaji na maafisa wa afya.

Serikali ya Syria imekana kutumia silaha za kemikali na kusema kuwa shambulio hilo lilipangwa ili kupata kisingizio cha kuishambulia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles