23.4 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Rais amtaka Messi kufuta kauli ya kujiuzulu

Lionel Messi
Lionel Messi

BUENOS AIRES, ARGENTINA

RAIS wa Argentina, Mauricio Macri, amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo, Lionel Messi, kwa lengo la kumuomba atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka katika timu ya taifa hilo.

Messi alifikia maamuzi hayo baada ya timu yake kushindwa kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za Copa America huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliokosa mikwaju ya penalti.

Messi alisema kwamba hawezi kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa kuwa ameshindwa kuisaidia kutwaa mataji makubwa katika fainali nne alizocheza, ikiwa mara tatu kwenye Copa America na Kombe la dunia.

Rais huyo amedai kwamba amefurahishwa na kiwango walichokionesha Argentina katika michuano hiyo ya Copa America, hivyo hakuna sababu ya mchezaji huyo kutangaza kujiuzulu kutokana na maneno ya watu.

“Nimeona fahari kwa kiwango ambacho Argentina wamekionesha katika michuano ya Copa America, hivyo sioni sababu ya Messi kutangaza kujiuzulu kwa kukosa kuipa ubingwa timu yake, hakuna haja ya kusikiliza maneno ya watu, ninamtaka aendelee kuitumikia timu hiyo,” alisema Macri.

Hata hivyo nyota wa zamani wa timu hiyo Diego Maradona, amemtaka Messi kuendelea kuitumikia timu hiyo ya taifa kwa ajili ya kuiongoza katika kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018 na anaamini ataweza kuipa ubingwa wa michuano hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles