27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Dani Alves ajiunga na Juventus

Dani Alves
Dani Alves

TURIN, ITALIA

BEKI wa timu ya Taifa ya Brazil, Dani Alves, amefanikiwa kujiunga na mabingwa wa Ligi Kuu nchini Italia, Juventus kwa mkataba wa miaka miwili.

Nyota huyo alikuwa anakipiga katika klabu ya Barcelona tangu mwaka 2008 akitokea klabu ya Sevilla kwa kitita cha Euro milioni 30, hivyo msimu mpya atakuwa chini ya kocha Massimiliano Allegri.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, ameondoka Barcelona baada ya kumaliza mkataba wake na hivyo alidai kwamba anaondoka kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu nchini Hispania kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya.

“Nimeondoka Barcelona kwa matakwa yangu mwenyewe, nilikua na furaha kwa miaka yote kutokana na kuvaa jezi ya klabu bora duniani, huku nikikutana na wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu, lakini kwa sasa nimepata sehemu nyingine ya kuendeleza maisha yangu ya soka na kupata changamoto mpya,” alisema Alves

Hata hivyo uongozi wa klabu ya Barcelona bado ulikuwa unahitaji huduma yake lakini mchezaji mwenyewe aliamua kuachana na klabu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles