31.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Rais akabidhiwa ripoti ya CAG

CAGNa Mwandishi wetu, Dar es Salaam

MDHIBITI na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG),Profesa Mussa Assad, jana alimkabidhi Rais Dk.John Magufuli taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Serikali ya mwaka 2014/2015, Ikulu  Dar es salaam.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa jana, ilisema Rais Dk. Magufuli alipokea taarifa hiyo yenye ripoti tano  ikiwa ni utaratibu wa katiba unaomtaka Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali,kukabidhi kwa Rais taarifa ya ukaguzi kabla ya mwisho wa   Machi.

“Baada ya kupokea taarifa hiyo, Rais Dk. Magufuli ataikabidhi mbele ya Bunge katika siku saba za mwanzo za kikao kijacho cha Bunge  mjini Dodoma,” alisema Msigwa.

Alisema Rais Dk.Magufuli amempongeza CAG na timu yake kwa kuandaa taarifa hiyo na ametoa wito kwa chombo hicho kuendelea kufanya kazi kwa uhuru na ufanisi, huku akiahidi Serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kufanikisha kazi zake.

Itakumbukwa katika Ripoti ya CAG ya mwaka 2014 iliyochunguza kashfa ya Tegeta Escrow, ilizua mjadala bungeni na kusababisha baadhi ya mawaziri akiwamo wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo, kujiuzulu.

Hata hivyo  inaelezwa ripoti ya sasa inaweza kuwa na viporo vya kashfa hizo na huenda ikafufua viporo vya kashfa zilizopita.

Katika ripoti ya mwaka 2012, Rais mstaafu Jakaya Kikwete alilazimika kulisuka upya baraza lake la mawaziri baada ya mawaziri kadhaa kuwajibishwa kutokana na kashfa za ubadhirifu wa fedha za umma.

Mawaziri ambao wizara zao zilibainika kuhusika katika vitendo vya ubadhirifu wa mali ya umma katika ripoti hiyo  na kulazimishwa  kujiuzulu ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Wengine ni  Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tamisemi, George Mkuchika.

Wengine ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige,   Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Haji Mponda na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk.Cyril Chami.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles