RAIS wa Misri, Abdul Fattah al-Sisi, amekosolewa vikali na raia wake baada ya kusema Serikali ina mpango wa kujenga gereza kubwa zaidi kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo.
Wakosoaji wameuona mpango huo kuwa ni upuuzi kwani Serikali ilipaswa kuelekeza nguvu katika ujenzi wa hospitali, shule, makazi ya watu na miradi ya maji.
Mmoja kati ya wananchi hao, Areej Algana, amesema: “Nimewahi kusikia marais wakizungumzia miradi ya hospitali, viwanda na sayansi lakini si ujenzi wa gereza. Hii ni mara ya kwanza kusikia.”
Haytham Abokhalil ni raia mwingine wa Misri aliyeungana na Algana akisema: “Haya ya gereza yanakuja huku kukiwa na uhaba wa hospitali na shule…”