28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

RAGHAV RAMJIT: BABA ALIYEPATA MTOTO AKIWA NA MIAKA 94

Untitled-1ANASEMEKANA kuwa ndiye baba mkongwe kuliko wote duniani, akiwa amejipatia mtoto wa kwanza aitwaye Bikramjeet wakati alipokuwa na umri wa miaka 94.

Mtoto wake wa pili Ranjeet alizaliwa miaka miwili baadaye, yaani wakati mzee huyu akiwa na umri wa miaka 96 huku mkewe Shakuntala Devi akiwa na umri wa miaka 61. Hiyo ilikuwa mwaka 2012.

Pamoja na uzee wake wote huo, Ramjit Raghav anadai kuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa mara tatu au nne kwa usiku mmoja.

Akizungumza nyumbani kwake katika jimbo la Haryana, kilomita 50 kutoka Delhi, Ramjeet aliongeza: “Mungu anipe nini? Huu ni utashi wa Mungu. Alitaka niwe na mtoto mwingine.”

Mstaafu huyo, ambaye anafurahia maisha na mkewe, walizaa wavulana hao wenye afya katika Hospitali ya serikali huko Haryana, Kaskazini mwa India.

Ramjeet ambaye anaishi katikia chumba kimoja, ana matarajio makubwa kwa wanae hao, akisema: “Nimekuwa mkulima kwa maisha yangu yote. Lakini ninataka wanangu wawe wafanyakazi wa ngazi ya juu serikalini.

“Imekuwa vyema kupata mtoto mwingine. Maana hata kama mmoja atafariki, Mungu aepushilie mbali, nitakuwa na mtu wa kuendeleza jina la ukoo wangu.”

Ramjeet alieleza namna madaktari walivyomcheka wakati aliposema amekuwa baba. Waliishia kucheka lakini walishangazwa walipobaini ukweli wa kile nilichomaanisha.”

Lakini pia alifichua kuwa majirani wake wamekuwa na wivu kuhusu urijali wake.

Ramjeet alisema: “Majirani zangu wana wivu na wamekuwa wakiuliza siri ya uwezo wangu lakini nawaambia ni mapenzi ya Mungu.”

“Nina afya njema na ninafurahia tendo la ndoa na mke wangu. Nadhani ni muhimu kwa mume na mke kufanya tendo la ndoa mara kwa mara kila inapobidi. Lakini kwa ajili ya mtoto wangu nimeweka hili kando kwa sasa.”

Baba huyo wa watoto wawili anadai kwamba ulaji wa kila siku wa vyakula  jamii ya karanga kama vile almonds, siagi za karanga na maziwa kunamfanya awe na uwezo wa kufanya tendo la ndoa kikamilifu.

Anadai kuwa anawashinda vijana wengi kwa uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa ukamilifu.

Anasema: “Namjali mke wangu na ninampatia kila kitu. Ni mwanamke mwenye furaha.”

Akizungumza namna alivyokutana na mkewe Shakuntala anasema; ilikuwa asubuhi moja mvua ikinyesha. Nilimkuta amekaa katika makaburi ya Kiislamu, nikamtaka twende nyumbani, akakubali na tangu hapo hakuondoka tena katika himaya yangu.

“Hakuwa na familia au marafiki na nilitaka kumsaidia,” alieleza.

“Nilimweka katika mbawa zangu na nilimfundisha yoga na tukaangukia katika penzi. Marafiki zangu wengi wa kike walifariki dunia na hivyo sikuoa tena na nikamuomba Shakuntala badala yake azibe pengo hilo, awe mke wangu.”

Shakuntala naye anaamini kuwa angekuwa ameshakufa kama si matunzo ya Ramjeet.

Alisema: “haijalishi umri wake, nampenda sana na ninamtunza vyema, ijapokuwa wakati mwingine ananikoromea.

“Haonekani kuwa mzee kwangu, anafanya tendo la ndoa sawa na mwanamume mwenye umri wa miaka 25 na hata kuwashinda kwa sababu anaweza kwenda usiku mzima, ni baba wa aina yake.”

Ndoa ya kwanza ya Ramjeet ni wakati akiwa na umri wa miaka 24 lakini baada ya kuwa mpweke kwa miaka 25 akaoana na mke wa sasa Shakuntala, ambaye wako pamoja kwa miaka 22 sasa.

Hata hivyo, mwaka mmoja tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto wa wa pili, pepo mbaya iliiangukia familia hii.

Ni baada ya uhusiano wa Raghav na mkewe kulegelega mapema mwaka 2013 wakati mwanao Bikramjeet alipotoweka wakati Devi alipokuwa amesinzia katika basi, alipoamka alikuta hayupo.

Baadaye Oktoba 2013, Devi aliamua kumuacha mumewe kwa kuondoka nyumbani akiwa na Ranjeet. Kabla ya mkewe kumuacha, Raghav alisema kwamba magenge ya wahalifu yamemteka mwanae huyo wa kwanza.

Licha ya kwamba alibakia kuchanganyikiwa, Raghav alieleza imani yake kwamba mkewe huyo atarudi nyumbani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles