PSG yamtaka Coutinho

0
782

philippe-coutinhoParis, Ufaransa

KLABU ya Paris Saint-Germain imemweka mchezaji wa Liverpool, Philippe Coutinho kwenye orodha ya wachezaji wanaotakiwa na klabu hiyo.

Mbrazili huyo (23), ni mchezaji muhimu wa timu ya Liverpool kutokana na uwezo wake akiwa uwanjani.

Alisaini mkataba wa miaka mitano Liverpool lakini tamaa ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya inaweza kubadili msimamo wake.

Coutinho kwa sasa anajiandaa na michuano ya Copa America inachezwa nchini Marekani akiwa na timu ya Brazili.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anatafuta saini ya Mario Gotze na Sadio Mane ili kuongeza nguvu katika timu hiyo.

Coutinho alisajiliwa na majogoo hao wa Anfield mwaka 2013 na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Brendan Rodgers, kwa mkataba wa pauni milioni 8 kwa mwaka akitokea Inter Milan ya Italia.

Mchezaji huyo alitua katika klabu hiyo akitokea timu ya Espanyol alipokuwa akicheza kwa mkopo ambako alikuwa akicheza chini ya kocha Maurcio Pochettino ambaye kwa sasa ypo Tottenham.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here