30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Profesa Safari: Chadema haijamaliza mamluki

Profesa Abdallah Safari
Profesa Abdallah Safari

NA ELIZABETH MJATTA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chadema Bara, Profesa Abdallah Safari, amesema hana uhakika kama wameweza kumaliza mamluki ndani ya chama hicho, bali wamejitahidi kuwadhibiti kupitia Uchaguzi Mkuu uliofanyika hivi karibuni.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili katika mahojiano maalumu, Profesa Safari ambaye aliwafananisha mamluki na kansa, alisema wanaweza kuharibu chama endapo watapata mwanya wa kufahamu mambo muhimu ya chama.

“Mamluki ni watu wabaya, nawafananisha na ugonjwa wa kansa (saratani), katika uchaguzi uliopita tumejitahidi kuwadhibiti ingawa siwezi kusema tumewadhibiti wote kwa sababu huwezi kujua, inawezekana ukamuona mtu ana dhamira nzuri na chama kumbe ni mtu mbaya, lakini inatosha kusema tumejaribu kuwadhibiti kwa kiasi kikubwa,” alisema Profesa Safari.

Alisema kwa sasa chama hicho hakiwezi kubabaishwa na mamluki kwani kimepita salama katika kipindi kigumu.

“Hiki chama kilipita katika kipindi kigumu sana, kipindi kile ambacho kina Kitila Mkumbo wameondoka ndiyo kilikuwa kipindi kigumu sana, toka niingie ndani ya hiki chama ndiyo nilishuhudia chama kikiyumbishwa, lakini tumepita salama, hatuwezi tena kutikisika,” alisema Profesa Safari.

Mwishoni mwa mwaka jana, Chadema ilipita katika wakati mgumu kuliko mwingine wowote baada ya kuwafukuza baadhi ya viongozi wake, wakiwatuhumu kwa usaliti kutokana na hatua yao ya kuandaa mikakati ya kufanya mabadiliko ya uongozi wakati utakapofanyika uchaguzi.

Baadhi ya watu waliotuhumiwa kuendesha mikakati hiyo ni aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu bara, Zitto Kabwe, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mkumbo na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Mwigamba na Kitila walivuliwa uanachama baada ya uongozi wa juu kudai umejiridhisha na madai dhidi yao ya kuandaa mikakati ya siri ya kukivuruga chama, huku Zitto akikimbilia mahakamani kuzuia hatua hiyo.

Soma mahojiano kamili kati ya gazeti hili na Profesa Safari Uk. 16 & 17.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles