Prezzo akumbuka alivyotoswa na Cash Money

0
953

prezzoNAIROBI, Kenya

NYOTA wa muziki nchini Kenya, Jackson Makini ‘Prezzo’, bado anakumbuka jinsi alivyotoswa na bosi wa kundi la Young Money Cash Money, Birdman, alipokwenda kuomba kujiunga na kundi hilo nchini Marekani.

Prezzo alitaka kujiunga na kundi hilo akidhani angekuwa mwakilishi kwa bara la Afrika, lakini bosi wa kundi hilo alikataa kwa madai kwamba msanii huyo wa Kenya hana kipato kikubwa kama wasanii wa kundi hilo.

“Nilifanikiwa kukutana na Birdman, lakini ilikuwa ngumu kupiga naye picha, lakini nilikutana na mtu anayefanana na Birdmani nchini Kenya nilipopiga naye picha wakadhani ndiye mwenyewe lakini haikuwa kweli walinitosa jamaa hata kupiga nao picha,” alisema Birdman.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here